Katika kizazi cha sasa idadi kubwa ya watu wanafikiri sana juu ya namna bora ambayo familia hasa watoto wao wanavyoweza kuwa na ustawi mzuri na maisha bora. Katika jitihada hizo ni familia chache sana zimekuwa na malezi sahihi yanayoendana na wakati. Kwa hiyo, familia nyingi zimepoteza uelekeo kuanzia kwenye msingi ambao ni malezi sahihi ya familia.
Sura zilizopo katika kitabu hiki.
1. Ijue Ndoa
2. Tendo la Ndoa kabla au nje ya Ndoa
3. Usijichagulie mwenzi wako
4. Namna ya kumpata mwenzi wako
5. Nini cha kufanya kama ulianza vibaya
Mwandishi wa toleo la kwanza la kitabu hiki, ni mwalimu ambaye amekuwa akifundisha masomo haya kwenye matamasha ya vijana, makanisa, makambi na sikukuu za vijana, akina mama na familia kwa ujumla. Kwa kweli ni mwalimu anayefaa hasa kuwaandaa vijana wanaoelekea kwenye maisha ya kujitegemea kiroho na kimwili. Mwandishi anaweza ana utayari wa pekee sana endapo atahitajika kwa semina za vijana, akina baba, akina mama na wanafamilia kwa ujumla. Pamoja na masomo hayo ni mwanandoa ambaye anaweza kuwambusha wanandoa kuhusu wajibu wao.
Mwandishi huyu, amethubutu kuweka kwenye kumbukumbu moja ya mafundisho muhimu kwa kanisa ambayo yanahitajika kwa wakati huu. Kwa njia hii pia, anawakumbusha na watu mbalimbali ambao wameelekezwa au kuguswa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu juu ya mambo kadha wa kadha na wakapuuzia, iwe ni fursa kwao pia kuthubutu kufanya kile walichoambiwa na kuweka kwenye kumbukumbu kwa ajili ya kizazi cha leo na kesho.
Ni maombi yangu kuwa kila anayesoma toleo hili apate kitu cha kumsaidia na kuwasaidia wengine ili tusipotee wote kwa kukosa maarifa