Kwanza kabisa, napenda kukiri kuwa mimi sina Elimu ya Theolojia,wala si mtaalamu wa mambo ya Dini ya Kikristo. Bali Neema ya Yesu Kristo ndani ya wokovu imenisukuma na kuniwezesha kujua siri za ndoa na kufundisha wengine kwa utukufu wake.
Mungu amenipa Neema kuifafanua elimu na maarifa ya Ndoa. Binadamu bila ndoa hajatoshelezwa hapa Duniani. Adamu alikuwa na kila kitu, akizungukwa na mazingira safi, Mungu akimtembelea kila wakati, bado hakuona utoshelevu. Alipokabidhiwa mke ndipo alipotulia na kutosheka kwa furaha kubwa mno na amani ya ajabu mno. Wanandoa wengi sasa hawaoni alichokiona na kukipata Adamu ndani ya Ndoa. Tuangalie kwanini Mungu amenisukuma kuandika kitabu hiki.
Ni msukumo aliokuwa ameuweka Mungu ndani ya Moyo wangu tangu mwaka 1996 juu ya Mwanzo bora wa Ndoa.
Kilio kilichoko ndani ya ndoa za watu wengi bila kujali Dini, Elimu, Cheo, Pesa na Umasikini iliendelea kunipa maumivu makali sana namna ya kumuuliza Mungu kwanini Ndoa.
Kutobadilika kwa urahisi pale wanandoa wanapofundishwa au kushauriwa au kupatanishwa, kulinipa maumivu zaidi.
Nikatambua kwa msaada wa Roho Mtakatifu kuwa, watu wengi hawaijui Elimu ya ndoa. Ndipo Mungu akaweka msukumo zaidi kuanzia mwaka 2010 kukiandaa kitabu hiki ili watu wajue kuwa Ndoa nyingi kwa asilimia kubwa zinaharibiwa kwa kutokuijua Elimu na Maarifa ya ndoa iliyomo ndani ya Biblia. Hivyo migogoro mingi iliyoko kwenye Ndoa kwa asilimia nyingi inasababishwa na mwanzo mbaya wa kutokujua nini Mungu amesema juu ya ndoa. Asilimia chache sana zinazobaki za migogoro ya wanandoa zinasababishwa na; Adui Shetani kupata mpenyo pamoja na Wanandoa kutojitambua.
Hivyo Mungu ameruhusu kitabu hiki ili ambao hawajaingia katika ndoa wajue namna wanavyotakiwa kuijua Ndoa ili waifurahie ndoa sawasawa na Ahadi ya Mungu.
Pili walioingia katika ndoa tayari, wajifunze namna walivyotakiwa kuijua Ndoa tangu mwanzo, hata ikiwezekana kutengeneza au kupatana na Mungu pale ambapo adui alipata uhalali kupitia mwanzo wao, vilevile waishi waitafute amani katika ndoa zao bila kuachana, kwani mtu akiijua ndoa hawezi kuanza vibaya wala aliyeko kwenye ndoa hawezi kuachana na mwenzi wake. AMINA.